Sunday, May 8, 2011

Baadhi ya watu waliompa Yesu maisha yao katika mkutano,wananyosha mikono yao juu kwa ishara ya kumweshimu Mungu...Biblia inasema ni furaha mwenye dhambi mmoja akitubu,nasisi tunaungana na mbingu kushangilia na kufurahi kwa kuokolewa kwa maisha yao..!Mungu awape neema ya kusimama.
Hakika mbele za Mungu wetu tuliserebuka katika ibada ndani ya kanisa Arusha ambapo TALITHA KUMI ministries ilikuwa ikihudumu.
Tuliserebuka kwelikweli mbele za Mungu katika Ibada Arusha.
Mtumishi wa Mungu Onjeni Njeni akihubiri katika Ibada iliyofanyika ndani ya kanisa la Jesus Healing Siwandeti Arusha,Mungu akubariki.
Mtumishi wa Mungu muimbaji Frank..akimsifu Mungu Arusha,Frank Mungu akubariki tumebarikiwa na huduma yako,kuja kwako Arusha si bure,Mungu atakutana na haja zako.Tunakupenda!Mungu akuinue katika utukufu mwingine.


Mungu alimuokoa binti Zawadi (katikati) ambaye alifungwa katika ushirikina kwa muda mrefu akitumiwa kama ajent kuvunja makanisa na kuharibu kazi za Mungu lakini alikutana na Mungu katika mkutano huo mkubwa wa injili huko Arusha,sasa ameokoka na anamtumikia Mungu.Yuko na watumishi wa Mungu wahudumu wa TALITHA KUMI Mery(kulia) na Itika(kushoto) wakimtia moyo.
Mtumishi wa Mungu Furaha Willy akihubiri katika mkutano mkubwa wa Injili huko Arusha,Mungu anamtumia kwa viwango vya juu sana,Mungu akubariki sana kaka.
Mchungaji kiongozi na mwenyeji wa kanisa la Jesus Healing Siwandet Arusha,mama Mery Shauri na mume wake Shauri,Mungu awabariki kwa kutupokea na kututunza vema kukiwa Arusha,tulijisikia nyumbani na tulibarikiwa pia.Tunawapenda.
Mtumishi wa Mungu Joshua Silomba akimsifu Mungu huko Arusha,Mungu akubariki Joshua
Wahudumu wengine aw TALITHA KUMI
Hawa ni baadhi ya wahudumu wa TALITHA KUMI,waliokuwa wakihudumu katika mkutano Arusha,Mungu awakumbuke kwa kujitoa kwenu...!
Baadhi ya viongozi wa TALITHA KUMI ,kutoka kushoto Mt.Filbert Francis,Wilikister,Edward,Deogratius,Onjeni,Furaha na Zakayo...Mungu awabariki kwa uongozi wao mzuri na Bwana atawalipa wasipozimia mioyo.
Baadhi ya wanakwaya wa (CASFETA) kutoka UDOM wakimsifu mungu ndani ya ibada iliyofanyika Arusha,Mungu awabariki ni kazi njema.
Baadhi ya watu waliohudhuria katika mkutano Arusha.

MATENDO MAKUU YA MUNGU ARUSHA

Mungu anaokoa hata wachawi,watumishi wa Mungu kutoka TALITHA KUMI wakichoma nguo za mchawi aliyeokoka...alizopewa na wachawi.

Monday, April 4, 2011


Mtumishi wa Mungu Furaha Willy akihubiri injili ya YESU KRISTO aliye hai siku ya kwanza ya mkutano.

Umati wa watu wakinyosha mikono yao juu kwa ishara ya kukabidhi maisha yao kwa YESU.

Mungu aliokoa watu mbalimbali katika mkutano na hawa ni baadhi ya watu walioamua kumpa YESU KRISTO maisha yao.Kwani neno la Mungu linasema YESU ndiye njia ya kweli na uzima, na mtu haji kwa baba pasipo njia ya YESU.yOH 14:6


Watumishi wa Mungu wakisikiliza mahitaji ya watu na kuwaombea.

Watumishi wa Mungu wakifanya maombezi kwa watu wenye shida na mahitaji mbalimbali.

Baadhi ya watu wakimsifu Mungu akiongozwa na Mwimbaji wa nyimbo za Injili Past.Beni


Makutano wakimwabudu Mungu aliye hai..

Wtumishi wa MUNGU wanaTALITHA KUMI wakiwa jukwaani wanamsifu Mungu wakiongozwa na Joshua Silomba(katikati).


Baadhi ya viongozi wa TALITHA KUMI wakiwa katika mkutano.

Baadhi ya watu waliohudhuria mkutano wakifuatilia kwa makini mahubiri.

Wapigaji wa muziki na mafundi mkitambo katika mkutano.


Baadhi ya watumishi wa Mungu wakliokuwa wakihudumu katika mkutano Arusha wakiwa katika jukwaa.

Mtumishi wa Mungu Deogratius Njeni akiomba kwa ajili ya mtumishi wa Mungu,


Mtumishi wa MUNGU Onjeni Njeni akihubiri wakati wa mkutano wa TALITHA KUMI huko ARUSHA

Wakati wa sifa watu wakijiachia vyema mbele za Mungu wao.maana hakuna astahiliye kusifiwa.

Mtumishi wa Mungu Muimbaji mwana TALITHA KUMI Frank Mbunda akiongoza ibada ya sifa.

Baadhi ya waumini wa kanisa la Siwandeti wakijibwaga wakati wa kipindi cha kumsifu Mungu.

Mtumishi wa Mungu Onjeni Njeni akifundisha maneno ya Mungu katika Ibada kubwa iliyofanyika katika kanisa la Siwandeti jijini Arusha.


Baadhi ya watu wliohudhuria katika ibada kanisani siku ya jumapili,ambayo ni siku ya kwanza ya mkutano.


Baadhi ya mafundi mitambo na wapiga vyombo vya muziki ambao ni watenda kazi ndani ya TALITHA KUMI.

baadhi ya watu wakimsifu Mungu katika mkutano wakati wa sifa.

Baadhi ya waimbaji wakimsifu Mungu siku ya kwanza ya mkutano, akiwemo Mwimbaji binafsi ENJOLIT KIMARO(katikati)

Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria katika mkutano mkubwa wa Injili siku ya kwanza huko Siwandeti Arusha.




Mchungaji kiongozi wa kanisa la Jesus healing Siwandeti Arusha mama Maria Shauri.


Watumishi wa Mungu Furaha Willy kutoka kushoto ambaye ni Katibu wa huduma ya TALITHA KUMI,na Onjeni Njeni ambaye nimwezeshaji mkuu (COORDINATOR) wa huduma ya TALITHA KUMI.

Mtumishi wa Mungu Edward Emanuel ambaye ni Mwenyekiti wa huduma ya TALITHA KUMI akiwa anamkaribisha mtumishi aliyeandaliwa kwa ajili ya neno siku hiyo.

Mchungaji na mama mchungaji Shauri,wenyeji wa kanisa la Jesus healing Siwandeti Arusha, ambapo mkutano Mkubwa wa Injili ulifanywa na huduma ya TALITHA KUMI.