
Wakati wa sifa watu wakijiachia vyema mbele za Mungu wao.maana hakuna astahiliye kusifiwa.

Mtumishi wa Mungu Muimbaji mwana TALITHA KUMI Frank Mbunda akiongoza ibada ya sifa.

Baadhi ya waumini wa kanisa la Siwandeti wakijibwaga wakati wa kipindi cha kumsifu Mungu.

Mtumishi wa Mungu Onjeni Njeni akifundisha maneno ya Mungu katika Ibada kubwa iliyofanyika katika kanisa la Siwandeti jijini Arusha.

Baadhi ya watu wliohudhuria katika ibada kanisani siku ya jumapili,ambayo ni siku ya kwanza ya mkutano.

Baadhi ya mafundi mitambo na wapiga vyombo vya muziki ambao ni watenda kazi ndani ya TALITHA KUMI.

baadhi ya watu wakimsifu Mungu katika mkutano wakati wa sifa.

Baadhi ya waimbaji wakimsifu Mungu siku ya kwanza ya mkutano, akiwemo Mwimbaji binafsi ENJOLIT KIMARO(katikati)

Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria katika mkutano mkubwa wa Injili siku ya kwanza huko Siwandeti Arusha.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Jesus healing Siwandeti Arusha mama Maria Shauri.

Watumishi wa Mungu Furaha Willy kutoka kushoto ambaye ni Katibu wa huduma ya TALITHA KUMI,na Onjeni Njeni ambaye nimwezeshaji mkuu (COORDINATOR) wa huduma ya TALITHA KUMI.

Mtumishi wa Mungu Edward Emanuel ambaye ni Mwenyekiti wa huduma ya TALITHA KUMI akiwa anamkaribisha mtumishi aliyeandaliwa kwa ajili ya neno siku hiyo.

Mchungaji na mama mchungaji Shauri,wenyeji wa kanisa la Jesus healing Siwandeti Arusha, ambapo mkutano Mkubwa wa Injili ulifanywa na huduma ya TALITHA KUMI.