Friday, April 1, 2011

KUHUSU TALITHA KUMI

       Ni huduma ya uamsho iliyoanzishwa mwaka 2007 mkoani Mbeya Uyole Tanzania,chini ya mwasisi wake Mtumishi wa Mungu Deogratius Njeni ambaye alipewa maono na Mungu wa mbinguni aliye hai, ambaye ndiye aliyepokea  wito wa huduma hii akishirikiana na wachungaji wa kanisa la Pentekoste Revival Church,akiwemo mchungaji Odiah Njeni na vijana wengine.
     Huduma hii ilipata mashiko zaidi mwaka 2010 katika Chuo Kikuu Cha Dodoma ambapo wanazuoni wengi walijiunga na huduma hii,na kuanza kumtumikia Mungu kwa kasi kubwa kwa kufanya huduma za mikutano ya nje,semina za ndani,ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba na mahubiri ya mitaani sehemu mbalimbali za nchi ya Tanzania na Mungu alionekana kitenda mambo makuu sana.


   

No comments:

Post a Comment