Sunday, May 8, 2011

Baadhi ya watu waliompa Yesu maisha yao katika mkutano,wananyosha mikono yao juu kwa ishara ya kumweshimu Mungu...Biblia inasema ni furaha mwenye dhambi mmoja akitubu,nasisi tunaungana na mbingu kushangilia na kufurahi kwa kuokolewa kwa maisha yao..!Mungu awape neema ya kusimama.
Hakika mbele za Mungu wetu tuliserebuka katika ibada ndani ya kanisa Arusha ambapo TALITHA KUMI ministries ilikuwa ikihudumu.
Tuliserebuka kwelikweli mbele za Mungu katika Ibada Arusha.
Mtumishi wa Mungu Onjeni Njeni akihubiri katika Ibada iliyofanyika ndani ya kanisa la Jesus Healing Siwandeti Arusha,Mungu akubariki.
Mtumishi wa Mungu muimbaji Frank..akimsifu Mungu Arusha,Frank Mungu akubariki tumebarikiwa na huduma yako,kuja kwako Arusha si bure,Mungu atakutana na haja zako.Tunakupenda!Mungu akuinue katika utukufu mwingine.


Mungu alimuokoa binti Zawadi (katikati) ambaye alifungwa katika ushirikina kwa muda mrefu akitumiwa kama ajent kuvunja makanisa na kuharibu kazi za Mungu lakini alikutana na Mungu katika mkutano huo mkubwa wa injili huko Arusha,sasa ameokoka na anamtumikia Mungu.Yuko na watumishi wa Mungu wahudumu wa TALITHA KUMI Mery(kulia) na Itika(kushoto) wakimtia moyo.
Mtumishi wa Mungu Furaha Willy akihubiri katika mkutano mkubwa wa Injili huko Arusha,Mungu anamtumia kwa viwango vya juu sana,Mungu akubariki sana kaka.
Mchungaji kiongozi na mwenyeji wa kanisa la Jesus Healing Siwandet Arusha,mama Mery Shauri na mume wake Shauri,Mungu awabariki kwa kutupokea na kututunza vema kukiwa Arusha,tulijisikia nyumbani na tulibarikiwa pia.Tunawapenda.
Mtumishi wa Mungu Joshua Silomba akimsifu Mungu huko Arusha,Mungu akubariki Joshua
Wahudumu wengine aw TALITHA KUMI
Hawa ni baadhi ya wahudumu wa TALITHA KUMI,waliokuwa wakihudumu katika mkutano Arusha,Mungu awakumbuke kwa kujitoa kwenu...!
Baadhi ya viongozi wa TALITHA KUMI ,kutoka kushoto Mt.Filbert Francis,Wilikister,Edward,Deogratius,Onjeni,Furaha na Zakayo...Mungu awabariki kwa uongozi wao mzuri na Bwana atawalipa wasipozimia mioyo.
Baadhi ya wanakwaya wa (CASFETA) kutoka UDOM wakimsifu mungu ndani ya ibada iliyofanyika Arusha,Mungu awabariki ni kazi njema.
Baadhi ya watu waliohudhuria katika mkutano Arusha.

MATENDO MAKUU YA MUNGU ARUSHA

Mungu anaokoa hata wachawi,watumishi wa Mungu kutoka TALITHA KUMI wakichoma nguo za mchawi aliyeokoka...alizopewa na wachawi.