Monday, April 4, 2011
MKUTANO MKUBWA ULIOFANYIKA ARUSHA TAR 6/3-13/3,2011
Mkutano huo uliofanyika Arusha kijiji cha Siwandeti wilaya ya Arumeru,ulihudhuriwa na watu wengi ambapo pia mungu alifanya mambo makuu, aliponya, aliokoa na mengine mengi Mungu wetu aliye hai alifanya.
Saturday, April 2, 2011
VIONGOZI WA TALITHA KUMI
Mkurugenzi wa huduma ya TALITHA KUMI,Mtumishi wa Mungu Deogratius Njeni kutoka Mkoani Mbeya Tanzania,ambaye ni mwanazuoni wa Chuo Kikuu Cha Dodoma mwaka wa tatu(mwisho) akichukua shahada ya Utawala wa Umma (BA,PUBLIC ADMINISTRATION).Huyu ndiye Mungu aliyempa kubeba maono ya huduma ya TALITHA KUMI
Friday, April 1, 2011
WAHUDUMU WA TALITHA KUMI
- Awe amempokea YESU KRISTO kama Bwana na Mwokozi wa maisha yake.
- Awe tayari kujitoa kwa ajili ya YESU KRISTO na si Mwanadamu.
- Awe amesajiliwa ndani ya TALITHA KUMI.
- Awe tayari kufuata Katiba na taratibu za TALITHA KUMI
NAMNA TALITHA KUMI INAVYOFANYA HUDUMA
TALITHA KUMI inafanya huduma kupitia njia mbalimbali kam vile:
- Semina za neno la Mungu ndani na nje ya kanisa.
- Mikutano ya Injili
- Warsha mbalimbali
- Mahubiri ya mitaani.
- Mahubiri ya nyumba kwa nyumba.
- Kutoa ushauri na kufanya maombezi kwa watu wenye mahitaji mbalimbali
MALENGO YA TALITHA KUMI
- Kutimiza neno la kinabii katika mpango wa YESU KRISTO wa kulijia na kulirejeza kanisa lake.
- Kuleta uamsho wa kanisa ulimwenguni kote kwa maana wakati wa Bwana na jeshi lake umetimia katika hatua katika hatua za mwisho za unyakuo wa kanisa .(Yoeli 1:15)
2.Kuinua vipawa vya Kimungu kati ya vijana kwa matabaka yote
3. Kukutana na jamii za watu mbalimbali wenye mahitaji maalum kama wagonjwa,walemavu,waathirika
wa UKIMWI na madawa ya kulevya.
MAONO YA TALITHA KUMI
TALITHA KUMI ina maono ya kufikisha Injili ya YESU kwa watu waliopo vijijini na mijini na kuwafungua waliofungwa na vifungo mbalimbali vya kiroho na kimwili {Isaya 61:1-2}
MAANA YA TALITHA KUMI
Ni huduma ya uamsho na urejesho wa vijana na watu wote.TALITHA KUMI ni neno la Kiebrania lenye maana ya KIJANA INUKA{Marko 5:41} ambalo lilitumiwa na YESU akionyesha wakati wa uamsho na ufufuo juu ya kanisa lake kama alivyoahidi katika kitabu cha Amosi 9:11,siku hiyo nitaiinua tene masikani ya Daudi iliyoanguka na kuziba kuziba mahali palipo bomoka,nami nitayainua magofu yake na kuyajenga kama siku za kale.
KUHUSU TALITHA KUMI
Ni huduma ya uamsho iliyoanzishwa mwaka 2007 mkoani Mbeya Uyole Tanzania,chini ya mwasisi wake Mtumishi wa Mungu Deogratius Njeni ambaye alipewa maono na Mungu wa mbinguni aliye hai, ambaye ndiye aliyepokea wito wa huduma hii akishirikiana na wachungaji wa kanisa la Pentekoste Revival Church,akiwemo mchungaji Odiah Njeni na vijana wengine.
Huduma hii ilipata mashiko zaidi mwaka 2010 katika Chuo Kikuu Cha Dodoma ambapo wanazuoni wengi walijiunga na huduma hii,na kuanza kumtumikia Mungu kwa kasi kubwa kwa kufanya huduma za mikutano ya nje,semina za ndani,ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba na mahubiri ya mitaani sehemu mbalimbali za nchi ya Tanzania na Mungu alionekana kitenda mambo makuu sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)